Huyu ndie aliyetabiriwa kuja kuwa mfalme baada ya ufalme wa Pele, Armando Maradona, Lionel Messi, na Cristiano Ronaldo. lakini alipangalo Mungu mwanadamu ni nani? apinge, basi huyu ndie Mwanamfalme aliyeshindwa kuwa mfalme, the prince who never become a
king.

Tarehe 23, ya mwezi october mwaka 1940 alizaliwa mfalme wa soka, huko nchini brazil aliyelitawala soka la Dunia kwa miongo miwili na kidogo Edson Arantes Nascimento almaarufu Pelé, mwaka 1975 Pele akiwa ameitumikia kwa miongo miwili, klabu maarufu brazil iitwayo Santos akaondoka klabuni humo na kuibukia new york cosmos alikocheza misimu miwili na kustaafu soka, tangu kipindi hicho Santos na brazil 🇧🇷 kwa ujumla haikuwa kushuhudia kipaji cha ajabu kama cha Pelé, santos ikasubiri kwa takribani miaka 8, kukishudia kipaji kingine halisi cha soka kutoka kwa Neymar da silva santos Junior.

Karibu katika makala safi ya mwanasoka wa kibrazil aliyezaliwa na kipaji cha kipekee, kipaji halisi cha soka, hapa tutazungumzia maisha yake ya ndani ya soka, mafanikio? kufeli nk. kama bado hujasubscribe channel yetu hii ya dino television fanya kusubscribe hapo then turn on notifications twende sawa, asante.

Neymar Da silva santos Junior, alizaliwa mwaka 1992 katika mji wa Mogi das Cruzes, jirani na sao paul huko nchini Brazil, nchi ambayo soka siyo tu kazi au burudani, bali ni utamaduni.

Neymar Tangu utotoni, alionyesha kipaji cha ajabu. Wakati wengine wakijifunza kutembea, yeye tayari alikuwa akidunda dunda mpira Baba yake neymar bwana Neymar Santos Sr., alikitambua kipaji chake mapema na kuanza kumfundisha soka taratibu, Baba yake, Neymar Santos Sr., ambaye pia alikuwa mwanasoka wa zamani, alitambua kipawa hicho mtoto wake akiwa na umri mdogo. Neymar alitumia masaa mengi akicheza mpira katika mitaa ya kawaida ya mtaa wake, akiwa na miaka saba tu baba yake akampeleka katika akademy ya
Portuguesa Santista, iliyokuwa karibu na kwao, Mpira ulikuwa kama sehemu ya roho yake, na mitaa ilikuwa jukwaa lake la kwanza.

Lakini maisha hayakuwa rahisi kila wakati. Kukua katika familia ya kawaida, Neymar alikabili changamoto ambazo zingeweza kumfanya mtu mwingine kukata tamaa. Familia yake ilikumbana na shida za kifedha, na shinikizo la kufanikiwa lilikuwa kubwa. Hata hivyo, upendo wa Neymar kwa soka haukudhoofika. Alikuwa akicheza miguu mitupu kwenye uwanja wenye vumbi, ndoto zake zikiwa kubwa kuliko vizuizi alivyokabiliana nazo. Mama yake, Nadine, mara nyingi alisimulia jinsi alivyokuwa akilia kila wakati alipofikishwa ndani, akiomba dakika tano zaidi na mpira.

Alivofika umri wa miaka 11 tu mwaka 2003, Neymar alijiunga na klabu ya santos, klabu ambayo pele alichukua ufalme wake wa soka,
Neymar alikaa kwenye academy ya santos mpaka 2009 alivyopandishwa timu ya wakubwa neymar akiwa na miaka 17 akacheza mechi yake ya kwanza ya kimashindano akaonesha kiwango cha juu kilichomfanya kocha kumuamini na kumpa nafasi mara kwa mara akaendelea kuitumikia santos kwa mafanikio makubwa, 2011 Neymar Alitunukiwa tuzo ya Mchezaji Bora wa ligi na akashinda Tuzo ya FIFA Puskás kwa jitihada binafsi kwenye ligi. Katika mwaka huohuo, aliisaidia Santos kushinda Copa Libertadores yao ya kwanza.
kipaji cha neymar kikaendelea kukua siku hadi siku mpaka njia zake zikaanza kufanananishwa na pele,
PelĂ©, ambaye mara nyingi alitajwa kama “baba” wa Neymar kwa uwezo wake wa soka, alimtazama kama mrithi wake. Lakini Neymar alikuwa na njia yake mwenyewe. Alipokuwa akikua, alishindwa kufanana na mafanikio ya PelĂ©, ingawa alikuwa na kipaji cha kutosha .

2013 kipaji cha Neymar kikawaka mpaka kikaonekana Camp Nou, nyumbani kwa lionel messi, Barcelona wakazama mfukoni na kutoa kiasi cha uero million 57, sawa sawa na billion 171 za kitanzania kwa rate ya sasa, Neymar akajiunga na barcelona akamkuta mfalme wa barcelona akiendeleza utawala wake laliga, neymar akaongezeka kwenye safu ya ushambuliaji ya barca 2014 barca wakamuongeza mwamba mwingine akitokea liverpool Luis Suarez, basi ndipo ule utatu mtakatifu ukatimia utatu wa Messi, Neymar na Suarez almaarufu kama MSN kipindi hicho wapinzani wao wana BBC Bale Benzema na Cristiano, usiombe ipigwe El classicico ilikuwa balaa tupu, basi bhana neymar akaitumikia barcelona kwa mafanikio makubwa akiisaidia timu kushinda michuano mbalimbali.
Neymar alibeba mataji mawili ya laliga, Uefa champions league moja, Copa de la rey1, Club world cup. na mengine kadhaa, pamoja na performance nzuri uwanjani Lakini majeraha yalikuwa adui wake mkubwa.

2017 matajiri wa paris Psg wakakiona kipaji cha neymar junior, nawakaweka nia thabiti ya kumnunua wakati huo
Barcelona ikiwa bado inamuhitaji zaidi lakini kama unavyojua pesa ni tamu kuliko asali, hakuna asiyependa kusikia habari zake, inapendwa na kila rika, kila kabila, kila taifa na kila mtu anavutiwa na kuhamasika pindi asikiapo habari za pesa basi bhana matajiri wa paris saint germain wakaweka mezani uero million 222 ambazo ni sawa na billion 666 za kitanzania kwa rate ya sasa hivi, Barcelona ni nani? Asimwachie neymar neymar akahama spain na kuingia France league 1, ambako huko alitumika Tangu 2017 hadi 2023 akiitumikia kwa mafanikio makubwa
Neymar alichukua mataji matano 5 ya france ligue 1
Copa de france 3
Copa de la league 2
Trophie de champion.

Lakini pia alifanikiwa kucheza fainal ya uefa cl 2020 ambapo psg walipoteza mbele ya bayern munich,
Pamoja na mafanikio hayo yote lakini bado majeraha yalikuwa yakimuandama back to back mpaka 2023 psg wakaamuuza kwa waarabu wa saudia, kwa euro million 97 sawa na billion 291 za kibongo, Neymar akaingia saudi pro league kwenye klabu ya Al hilal akasaini kandarasi ya miaka miwili huko alizioga fwedha, alikula mahela, ngwawira akawa anakula salary ya euro million 2.5 kila week yaani sawa na Bilioni 7.5 imagine ni week hio mwezi ni B 30 duuh mfano ukapewa wewe ungefanyia nini? Hela zote hizo.
Sasa huku ndio injury zikazidi tangu alivojiunga na Al hilal hakuwai kuitumikia al hilal ata kwa nusu msimu, kwa sababu ya majeruhi ya kila mara, kuna muda alikaa muda mrefu akiuguza majeraha baadae akarudi baada ya wiki mbili tu, alivojiunge tenah na kikosi cha al hilal, katika mechi ya kwanza neyma aliingia dakika ya 57 ya mchezo akitokea benchi kwenye mechi ya Afc Champions league dhidi ya Esteghlal hakucheza dkk nyingi dkk ya 86 tu akatolewa baada ya kupata majeraha tenah, daah basi bhana msimu wa mwisho ulivomalizika Al hilal nao wakamalizana na neymar. Akabaki anasubiri dili lingine.

Kama ilivyo kwenye maisha kuna wakati, Utakataliwa kila sehemu, kuna wakati watakuchafua kila mahali, kuna wale waliokuwa wakikukubali kisa mali, umarufu wako ama vingenevyo, wakati vikipotea watakupotea bila kujali lakini, kumbuka kuna Nyumbani, nyumbani ndio mahala pa mwisho lilipo tumaini lako ambapo kila mtu atakupokea huko, haijalishi ni nini? umepitia, haijalishi mabaya au shida kiasi gani ulizonazo lakini Nyumbani kutabaki kuwa nyumbani
basi neymar Junior dos Santos baada ya kuona kila sehemu hatakiwi, kila klabu ikifikiria kumsajili inaona hasara maana muda wowote anaweza kupata injury na asiitumikie klabu ipasavyo, wengine wakijisemea Neymar ni mchezaji mzuri ila shida injury, hatununui vilema sisi, basi Neymar akaikumbuka ile kauli ya nyumbani ni nyumbani hata kama ni shambani, japo nabii hakubariki kwao, ila mcheza kwao hutuzwa, na sikuzote zimwi likujualo halikuli likakwisha,
Baada ya miaka 12, mwamba akaamua kurudi nyumbani, sehemu kilipozikwa kitovu chake, katika ardhi ya Sao pauli kusini mwa Brazil, neymar akarudi katika timu yake ya utotoni mahali aliposhika mpira kwa mara ya kwanza, mahali alipojulia kupiga vyenga vya maudhi, sehemu iliyomkuza kimwili, kiroho mpaka kiakili, Santos football club, Naam wazazi wake wa football wakampokea tenah, mwanamfalme wa soka. wakamwambia kijana hapa ndipo nyumbani karibu nyumbani. basi bhana tarehe 18 February 2025 Neymar akasaini kandarasi ya miezi 6 ya kuitumikia klabu ya yake hio ya zamani, na mapokezi yake yanatajwa kuwa watu wapatao elfu 20 katika uwanja wa Belmiro walipata kuhudhuria tafrija ya kumkaribisha tenah mwana mfalme wa soka Neymar Junior dos Santos. Neymar alipopewa nafasi ya kuzungumza mbele ya umati wa mashabiki hakuwa na mengi ya kusema. Basi bhana akaendelea kukipiga santos baada ya mechi kadhaa akapata injury tenah. Mpaka sasa amecheza michezo 7 pekee akiwa na santos akifunga magoli matatu na asists tatu.

Hebu tuangazie maisha yake ya soka la kimataifa, Neyma junior aliitwa kwa mara ya kwanza katika timu ya vijana ya brazil Under 17 mwaka 2009, baada ya kutimiza miaka 18 akaitwa timu ya wakubwa kwa mara ya kwanza tokea hapo akawa anaitwa mara kwa mara

Neymar amecheza kombe la Dunia mara 3,
Neymar ndie Top scorer of all time ( yaani mfungaji bora wa muda wote wa timu ya taifa ya brazil akiwa na magoli 79.
2013 alishinda fifa confederation cup akiwa na brazil lakini pia
Ana medal ya dhahabu ya Rio 2016. Katika Olympic.
Neymar ni moja ya wachezaji wenye mafanikio mengi sana katika soka, pamoja na injury zote ila bado
Neymar yupo kwenye orodha ya wachezaji waliowahi kufunga magoli mengi, kwenye maisha yao ya soka. Katika mechi 717 alizocheza katika maisha yake ya soka Neymar amaefunga magoli 439. Imajini isinekuwa mambo ya majeraha jamaa angukua na ballon d’or ngapi? Kabatini.

Ama kweli, He is A prince who never became a king

Neymar hakuwahi kuwa mfalme wa soka, lakini alikuwa na hadithi ya kipekee. Alipigana na majeraha, matarajio makubwa, na mazingira magumu, lakini alibaki kuwa mchezaji wa kuvutia na mwenye kipaji kikubwa sana.

hayo yalikuwa ni maisha ya ndani soka ya Neymar Junior embu tuangazia kidogo maisha yake ya nje ya soka.

Neymar si mchezaji wa soka pekee; pia ni mpenzi wa michezo ya video, yaani Video Games anacheza sana play stations, na Ana uhusiano wa karibu na ulimwengu wa eSports, na mara nyingi huonekana akicheza Fortnite au CS:GO kwenye mitandao ya twitch. Mwaka 2020, alianzisha timu yake ya eSports, Neymar Jr. Esports Team

Mbali na kuwashangaza watu uwanjani, Neymar ni mtu wa kujitoa sana katika maswala ya kijamii.

Mwaka 2014, alizindua shirika la Instituto Neymar Jr. huko Praia Grande, Brazil, lenye lengo la kusaidia watoto wenye mahitaji katika elimu, michezo, na fursa za kiafya. Mpango huo umesaidia zaidi ya watoto 10,500 na familia zao,
Hata wakati ambao alipata lizikizo za majeruhi katika soka, basi mara kadhaa alionekana akiwa karibu na watoto wenye mahitaji maalumu, akionyesha upendo wake wa kina kwa watoto hao.

Neymar ni mwanamitindo wa asili eeh, yaani ni kwamba mwamba hajawahi kusomea mitindo ila Ana sifa ya kuvutia kwenye mitindo yake mbalimbali—
mara kadhaa utakuta ameziweka rangi nywele zake, na huziweka katika staili mbali mbali, kitu ambacho kinawavutia hadi wachezaji wanaochipukia, nyota wa sasa wa klabu ya Barcelona bwana mdogo Lamine Yamal katika moja ya mahojiano yake, aliwahi kusema anakubali style za nywele hata uchezaji wa neymar Junior. gold katika nywele zake

ukiacha kuwa neymar ni mchezaji aliyetengeneza pesa nyingi sana katika soka lakini ametengeza pesa nyingi pia katika Endorsement za brands Neymar amekuwa balozi wa makampuni makubwa Duniani,
Neymar amewahi kuwa balozi wa kampuni kubwa za vifaa vya michezo Kama NiKe, Jordan na kwa sasa anafanya kazi na Puma,
ukiachana na endorsement za makampuni ya vifaa vya michezo Neymar pia amefanya kazi na anaendelea kufanya kazi na Brands nyingine nyingi tu tofauti kama Beats Electronics, EA Games, Gillette, MasterCard. McDonald’s, Red Bull, na REPLAY JEANS, BLAZE BET nk. ukiacha kufanya kazi na brands mbali mbali Neymar ana brand yake ya mavaziana iitwayo NJr ambayo inauzwa kwa mashabiki. kwahiyo neymar kwake fashion ni maisha.

Ukizungumzia watu wanaozipenda familia zao, basi neymar anaupendo mkubwa sana kwa familia yake Ana uhusiano wa karibu sana na baba yake mzazi, Neymar Santos Sr. (ambaye pia ni meneja wake), mama yake Nadine, na dada yake Rafaella. Rafaella, ambaye ni mwanamuziki na blogerr maarufu brazil. mara nyingi Neymar kila mwisho wa mwaka hufanya mtoko wa kifamilia.
Neymar ni babaa watoto watatu kila mtoto ma mama yake, Mwanawe wa kwanza ni wa kiume aitwae Davi Lucca (aliyezaliwa 2011), aliyempata kwa aliyekuwa girlfriend wake Carolina Dantas, mwanae wa pili ni wa kike anaitwa Mavie mama yake anaitwa Bruna Biancardi, na wa mwisho ni wa kike aitwae Hellen alimpata mwaka wa jana 2024. kwa Amanda Kimberlly, mwaka huu amerudiana tenah na mama wa mtoto wake wa pili Bruna biancardi na wanatarajia kupata mtoto mwingine hivi karibuni maana bdada huyo ni mjamzito kwa sasa. na wawili hao wako mbioni kufunga ndoa ya kanisani.

pamoja na kuwa na mahusiano hio haimzuii Neymar kukutana na wanae hao wengine, amekuwa na utaratibu wa kukutana na watoto wake wote katika baadhi ya mechi, Neymar hupenda kutumia wakati mwingi na mtoto wake,
mtoto wake wa kwanza Davi Lucca anapenda kucheza mpira na anasoma Barcelona’s Escola school, shule ya ball ya barcelona ambapo watoto wakitoka hapo wanajiunga na academy kuu ya Barcelona La masia academy,

Neymar ni mtu wa watu neymar yupo miongoni mwa wale wachezaji wenye 0 hatters, yaani ukimchukia neymar basi umeuchukia na mpira wenyewe, neymar ni rafiki wa watu wengi. mashuhuri, kama kina Lionel Messi na Kylian Mbappé, Vini jr , raphinha, Rodrygo, Suarez, Lamine yamal lakini pia hana baya pia Cr7 ni mtu wa watu huyu mwamba.

Watu wengi husema kipindi cha ujana wake aliponda sana raha, umaarufu ulimuendesha kwa kiasi, na wengine hufika mbali na kusema kuwa huenda hata injury alizokuwa akizipata kwenye mpira ni sababu ya kula bata na kuwa mvuvi wa mazoezi,

Neymar pia ni mpenzi wa muziki. Ameshiriki katika video za muziki za wasanii kama Sertanejo na Funk Brasileiro, na mara kadhaa hutembelea studio za music Alishiriki kwenye wimbo wa MC Kevinho, “Tudo Ok”, akionyesha uwezo wake wa kuimba na kucheza densi. Mara nyingi neymar amekuwa akiarikwa kwenye matukio makubwa ya mziki kama tuzo mbalimbali kama vile grammy katika miji kama Paris, Miami, au Rio dijeneiro.

Neymar Aliwahi kukabiliana na kashfa za kukwepa kodi serikalini, mashtaka ya ubakaji (ambayo alikataa na kusitishwa mwaka 2021),

Ukiachilia mbali, Ubishoo wake, Tatoos zake mwilini neymar ni mtu wa imani sana, pamoja na mali umaarufu aliokuwa nao lakini anaamini kuwa fedhe, dhahabu, umaarufu, maisha mazuri vyote hutoka kwa Mungu, kwahiyo anaikumbuka vyema nyumba ya ibada siyo tu wakati wa matatizo bali hata wakati wa raha, neymar toka utoto wake alipenda kwenda kanisani mpaka leo, Neymar ni muumini mzuri dini ya kikristo, neymar huamini katika yesu kristo hata alivyokuwa mdogo wakati akiitumikia academy ya santos alipenda kufunga kitambaa kichwani chenye maandishi ya 100% Jesus hata hivi karibuni alivyorejea kwa mara ya pili klabuni hapo wakati wa utambulisho wake alifunga kitambaa hicho cha 100% Jesus katika paji lake la uso, lakini pia alipokabidhiwa locker yake ya jezi aliweka kitabu kitakatifu cha biblia na alipiga goti na kufanya Dua katika Locker yake.

Neymar ni mtoto wa kiBrazil aliyepambana kwa hali na mali kufanikiwa katika soka, neymar ni mtoto mwenye Familia yenye upendo, na mjasiriamali mwenye ndoto. Anaamini kuwa “maisha ni mchezo mzuri zaidi kuliko soka lenyewe.”* Asante kwa kunisikiliza dodosha comment yako hapo kwenye comment kama ulikuwa sambamba na mimi mwanzo mpaka mwisho, fanya kusubscribe kama bado hii hapa ni supa 12 ya dino television mi naitwa Dennis Dinomineta tukutane tenah panapo majariwa yake mwenyewezi Mungu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *