![]()
Kuna tofauti kubwa kati ya kucheza mpira, na kubeba matumaini ya mamilioni ya mioyo ya watu.
Kombe la Dunia la mwaka huu, siyo tu mashindano ya soka, hii ni vita ya mwisho ya kihisia, ni karata ya mwisho, ndio tumaini pekee lilobaki kwa malegend wengi wasoka.
Hawa ni mastaa kumi (10) ambao hawachezi tu kwa ajili ya nchi zao,
bali kwa ajili ya mamilioni ya wafuasi ulimwenguni kote, wanaoomba usiku na mchana kuona mashujaa wao wanaondoka jukwaani kwa heshima kuu.
Kutoka Buenos Aires hadi Lisbon, na hata hapa kwetu Afrika, mamilioni ya wafuasi wanatamani kuona miungu hawa wa soka wakiondoka kwa tabasamu.
Kwa Cristiano Ronaldo, mashabiki wake duniani kote, wanaamini hili ndilo litakalo kuwa kombe lake la kwanza na la mwisho la Dunia kunyanya, wanamini kwamba atarudi nyumbani akiwa na hili kombe, kombe pekee lililomkataa kwa mara tano toka aanze kulisaka mwaka 2006, ingekuwa kombe hili linatolewa kama zawadi basi huyu mwamba angestahili kupata kwasababu ya mafanikio makubwa ambayo ameweza kuyaonesha katika soka, huyu ndie mwanasoka mwenye ushawishi mkubwa zaidi duniani, kashinda makombe 35 katika maisha yake ana kila kombe unalojua kubwa, ballondor za kutosha, mchezaji mwenye magoli mengi zaidi kwa sasa anaikaribia rekodi ya magoli elfu moja, mchezaji aliyelitumikia soka kwa zaidi ya miongo miwili kwa mafanikio makubwa lakini hayo yote yanaonekana kama hakuna alichofanya kwasababu tu ya kukosa worldcup. kama kuna ombi atakuwa analiomba sana kwa wakati huu bwana Cr7 ni kuchukua hili kombe la dunia.
Nchini Brazil, soka si tu mpira wa miguu ni dini, na NEYMAR JUNIOR ndiye mtume wao. ukiwazungumzia wachezaji wa kizazi cha kuanzia 2000s wenye mafanikio mengi kwenye soka basi baada ya Messi na Ronaldo ni neymar Jr
Wafuasi wake pande zote za dunia wanajua fika kuwa amebeba presha ya kuwaletea kombe ambalo Brazil haijaligusa tangu mwaka 2002, richa ya kuwa Brazil 🇧🇷 ndiyo nchi yenye makombe mengi ya dunia katika historia lakini kwa neymar Junior hajawahi kubahatika kubeba kombe la Dunia, na hili linaenda kuwa kombe lake nne na kila mmoja anatamani mwisho mzuri kwa kipaji hiki kilichoteseka sana na majeraha.
Hapa nyumbani Afrika, machozi na matumaini ya bara zima yapo kwa Mohamed Salah na Sadio Mané. hawa ndio wachezaji bora wa afrika kwa miaka ya hivi karibuni, wameipeperusha vyema bendera ya africa barani ulaya kwa zaidi ya muongo mmoja bado majina yao yamekuwa ya kisumbua duniani,
Wafuasi wao kote duniani hawataki tu kuona wakicheza, wanataka kuona mmoja wao akivunja mwiko na kurudisha Kombe la Dunia kwenye ardhi ya Afrika kwa mara ya kwanza kabisa katika historia. Kwa upande wa Sadio Mané, yeye mwenyewe amesharekodiwa akisema hili ndilo Kombe lake la mwisho kabla ya kustaafu soka la kimataifa, hivyo mashabiki wake wana kiu ya kuona Simba huyu wa Teranga haondoki kinyonge. Mané amepata bahati ya kucheza mashindano ya fainali za Kombe la Dunia mara moja tu katika maisha yake yote ya soka hadi sasa.
2018 Mané alicheza mechi zote 3 za hatua ya makundi dakika zote 270. Alifunga goli lake la kwanza na la pekee la Kombe la Dunia katika sare ya 2-2 dhidi ya Japan kwenye hatua ya makundi. 2022 akalikosa kombe la dunia kwasababu ya Injury. so hii ndio last dance kwake.
mashabiki wa Mancity, napoli na wabelgiji, wanatamani kumuona fundi Kelvin De Bruyne (KDB) akipata mwisho mzuri kama wa kwenye hadithi za kale, kwa sababu ulimwengu unajua soka lake la kiungwana na ubunifu wake unastahili heshima ya dhahabu. zaidi ya miaka 14 kwenye ligi zenye ushindani mkubwa, akibeba mataji zaidi ya 24 makubwa, akiweka rekodi nyingi na kubwa lakini kombe la dunia hajawahi kulinusa katika maisha yake ya soka
Msimu mzuri zaidi wa Kevin De Bruyne (KDB) kwenye Kombe la Dunia bila shaka ulikuwa wa mwaka 2018 nchini Urusi (Russia 2018).
​Katika michuano hiyo, KDB aliongoza kizazi cha dhahabu cha Ubelgiji kufikia mafanikio makubwa zaidi katika historia ya nchi hiyo kwenye Kombe la Dunia.
Ubelgiji ilimaliza katika nafasi ya tatu baada ya kuifunga Uingereza 2-0 kwenye mechi ya kusaka mshindi wa tatu. Haya yalikuwa mafanikio makubwa zaidi ya taifa hilo tangu walipomaliza nafasi ya nne mwaka 1986.
Hii ndiyo mechi inayokumbukwa zaidi msimu huo. KDB alicheza kama “False 9” au mshambuliaji wa mbele chini ya kocha Roberto MartÃnez, mbinu iliyowashtua sana Brazil. Alifunga goli la pili kali sana la shuti la mbali lililoisaidia Ubelgiji kushinda 2-1 na kutinga nusu fainali, na alitunukiwa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mechi (Man of the Match).
Son Heung-min Kipenzi cha bara la Asia, Son Heung-min, ana wafuasi wengi sana si tu Asia lakini kote duniani, akitajwa kati ya wale wachezaji wenye zero heaters, wengi wanaompenda kwa unyenyekevu wake, na kila mtu anatamani kuona akiondoka uwanjani kwa tabasamu kubwa na sio kwa machozi ya huzuni.
Luka Modrić mfalme wa croatia ðŸ‡ðŸ‡· baada ya kulikosa kombe hili kwa mara nne sasa, ni mwaka wake wa tano anakwenda kulitafuta, mwaka 2018 ndio mwaka bora sana kwake katika kombe la Dunia, kwa mara ya kwanza timu yake ya taifa iliingia fainal ya kombe la Dunia na kwa bahati mbaya ikapoteza fainal kwa goli 4 kwa 2 dhidi ya timu ya taifa ya ufaransa. luka Modric akifanikiwa kuondoka kama mchezaji bora wa mashindano akipewa tuzo ya golden ball. mara ya mwisho tumemshuhudia kombe la dunia la mwaka 2022 ambapo timu yake ya Croatia ðŸ‡ðŸ‡· walimaliza kama washindi watatu baada ya kutolewa na arigentina nusu fainal na baadae wakamfunga Morocco 🇲🇦 katika kutafuta mshindi watatu, kwahiyo pamoja na kuwa amebeba karibu kila kombe duniani akiwa na uefa 6, makombe ya ligi na mataji mengi yanayotajwa kufika 28, bado taji kubwa na muhimu worldcup amelikosa, na hili litakuwa kombe lake la 5 kucheza, kwahiyo matumaini yote yako hapa, hii ndiyo karata yake ya mwisho.
Kuelekea Kombe la Dunia la mwaka huu, hatuombei tu timu zetu zishinde, tunaombea hisia za mamilioni ya watu zisivunjike vipande vipande. Hawa wachezaji wametuondolea stress za maisha kwa miaka 15, na sasa tunataka kuona wakiondoka kama wafalme. Wewe shabiki wa soka, ni star gani kati ya hawa unayeomba usiku na mchana abebe hili kombe na kupata mwisho mzuri? Shusha comment yako sasa hivi, na usisahau ku-follow akaunti hii kwa dondoo zaidi za hisia za soka.
